Monday, 23 March 2020

AFYA: TABIA ZINAZOWEZA KUHARIBU UTENDAJI KAZI WA FIGO ZAKO


Matumizi mabaya ya dawa za maumivu (painkillers): Ni kweli utumiaji wa dawa hizi unaweza kukusaidia kwa kukuondolea maumivu lakini unapozitumia kila wakati bila ushauri mzuri kutoka kwa wataalam wa afya huweza kuleta madhara kwenye figo

-
Kutokunywa maji ya kutosha: Kunywa maji mengi husaidia figo kujisafisha, kuondoa sumu mwilini na ni njia mojawapo ya kukwepa kupata mawe kwenye figo (kidney stones). Unashauriwa kunywa angalau lita 2 za maji kwa siku
-
Matumizi makubwa ya vyakule vyenye sukari: Sukari inachangia kuongezeka uzito na kukuweka kwenye hatari ya kupata shinikizo la damu na Kisukari, ambazo hizi ni sababu ziletazo matatizo kwenye figo. Kuwa makini na sukari inayopatikana kwenye bidhaa zilizosindikwa
-
Baadhi ya dalili za kuwa na tatizo kwenye Figo ni pamoja na kujisikia uchovu sana na mwili kutokuwa na nguvu, kukosa hamu ya kula na kupata shida katika kupata usingizi, ngozi kuwa kavu sana, macho na miguu kuvimba hasa unapoamka asubuhi na kushikwa na haja ya kukojoa mara kwa mara, haswa usiku

No comments:

Post a Comment